Thursday, 3 September 2015

MAISHA YANGU SEHEM YA TATU

ILIPOISHIA....

Kesho yake asubuhi nilikaa na mara nuru akasogea karibu yangu na kumuuliza ehe niambie ile ishu uliotaka kuniambia kuhusu mchongo wa pesa.
inaendelea.

Baada ya nurdini kuumuliza hivyo alikaa kimya na kuniangalia kwa makini halafu akasema"usistuke sasa nikikwambia ishu yenyewe"
kwa shangwe nikajibu "sawa sitastuka we sema tuu"

Nurdini akajiweka vizuri halafu akaangalia kulia na kushoto kwa makini halafu akaanza kuongea
"ujue nini kuna mpango nimeuwaza tuufanye halafu tukimbie hapa kijijini"
nikadakia
"mpango gani huo"
nurdini akasema "acha mapepe wewe subiri nimalize kuongea huku akiwa anageuka huku na huku
akaendelea "tukishafanya huo mchongo tunakimbia mbali na kijiji hichi. Akameza mate huku mimi nikiwa kimya namsikiliza kwa makini,akaendelea hiyo ishu unahusu pesa za kijiji,
nikihamaki "pesaaa za kijijiiiii kivipiiiii..../!,nrdini alinyanyuka na kusema mbona unafoka sasa kama sio mwanaume jasiri bwana jikaze wewe kama vipi tughairishe,nikanywea basi rudi nurdini usikasirike bwana.

No comments:

Post a Comment